Sunak azindua mpango wa kupiga marufuku matumizi ya sigara za kielektroniki

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak

Uingereza itaanzisha sheria ya kupiga marufuku matumizi ya sigara za kielektroniki ili kukabiliana na ongezeko la uvutaji kwa vijana, haya ni kwa mujibu wa Waziri Mkuu Rishi Sunak ambaye alitangaza leo Jumatatu.

Sigara za kielektroniki, zinazojulikana kama "puffs", zinapendwa na vijana, zinaweza kuwa na dawa aina ya nikotini ya juu, inayowekwa ladha tofauti na ni bei nafuu.

Serikali ilitoa takwimu za hivi majuzi zilizoonyesha idadi ya watumiaji wa sigara hizo walio chini ya umri wa miaka 18 wanaotumia sigara hizo imeongezeka karibu mara tisa katika miaka miwili iliyopita

Serikali ya Sunak pia inapanga kuanzisha faini kwa maduka nchini Uingereza na Wales ambayo yanauza vapes kinyume cha sheria kwa watoto.

Wataalamu wa afya walikaribisha pendekezo hilo, huku Afisa Mkuu wa Matibabu Chris Whitty akisema sheria hiyo itakuwa na "athari kubwa ya afya ya umma katika vizazi vingi vijavyo".

Chris Whitty

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP