Hilo huenda likawa pigo kubwa kwa sera kuu ya serikali ya Waziri Mkuu Rishi Sunak ambayo imeangaziwa sana kimataifa na kukosolewa. Majaji watano katika mahakama ya juu walitoa kwa kauli moja kuwa wale wanaoomba hifadhi kupelekwa nchini Rwanda itakuwa ni ‘kutendewa vibaya’ kwasababu huenda wakarejeshwa katika nchi zao walizozikimbia.
Sunak ambaye aliahidi kusitisha wimbi la wahamiaji kufika nchini Uingereza kwa kutumia boti ndogo ndogo wakivuka eneo la English Channel, amesema maamuzi hayo si matokeo ambayo aliyataka.
Uamuzi wa leo ndiyo wa karibuni zaidi kwenye mvutano ulioanza Aprili mwaka jana baada ya Uingereza kutia saini mkataba na Rwanda kwa kutuma wahamiaji wasio na stakabadhi kwenye hifadhi za muda kwenye taifa hilo la mashariki mwa Afrika.
Forum