Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 06:55

David Cameron wa Uingereza ndiye Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza kwa sasa


David Cameron ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza.
David Cameron ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza.

Kurudi kwa Cameron inaelezewa kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak anataka  kumleta mtu wa mrengo wa kati zaidi, mwenye uzoefu badala ya kuwatuliza mrengo wa kulia katika chama chake ambao walimuunga mkono Braverman. 

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amemrejesha madarakani kiongozi wa zamani David Cameron kama waziri wa mambo ya nje katika mabadiliko yaliyosababishwa na kutimuliwa kwa waziri wa mambo ya ndani, Suella Braverman baada ya ukosoaji wake dhidi ya polisi kuwa wanatishia mamlaka yake.

Ni hatua ya hivi karibuni kwa Waziri Mkuu ambaye chama chake cha Labour kinafanya vibaya kabla ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao. Kurudi kwa Cameron inaelezewa kuwa Sunak anataka kumleta mtu wa mrengo wa kati zaidi, mwenye uzoefu badala ya kuwatuliza mrengo wa kulia katika chama chake ambao walimuunga mkono Braverman.

Pia inaamsha mjadala wa mgawanyiko juu ya Brexit; Cameron alifanya kura ya maoni juu ya uanachama wa Umoja wa Ulaya katika mwaka 2016 na alichukiwa na wengi wa mrengo wa kulia katika chama baada ya kufanya kampeni ya kubaki. Alijiuzulu saa chache baada ya Uingereza kupiga kura ya kujiondoa.

Forum

XS
SM
MD
LG