Madaktari wanaoshiriki katika mgomo huo walimiminika nje mtaani huko Nottingham, Birmingham, Newcastle na Liverpool kanda za video zimeonyesha.
Kama ilivyo katika sekta ningine katika muda wa mwaka mmoja uliopita, madaktari hao wadogo waliwakilishwa na British Medical Association BMA wamefanya mfulululizo wa migomo kudai malipo mazuri huku mfumuko wa bei ukiendelea kupanda.
Katika taarifa, umoja huo umeisihi serikali kutoa ‘ombi la uhakika’ la malipo ili kumalia migomo, ambayo inatishia kuongeza shinikizo kwa huduma za afya, ambako zaidi ya watu milioni 7.7 wako katika orodha ya kusubiri matibabu.
Kwa ujumla, NHS ambayo imetoa huduma za afya bure tangu ilipozinduliwa mwaka 1948, imefuta uteuzi wa takriban nafasi milioni 1.2 tangu migomo ilipoanza mwaka 2023.
Serikali, ambayo imekubali makubaliano ya malipo mapya na wafanyakazi wengine wa huduma za afya, wakiwemo wauguzi na madaktari waandamizi katika miezi ya karibuni, wamesita kuongeza malipo wakisema itaongeza hali mbaya ya mfumuko wa bei.
BMA imeacha mazungumzo na serikali baada ya kupewa ombi la ongezeko la asilimia 8 na 10 ya malipo, na kuitisha migomo kuanzia Desemba 20 mpaka 23. Umoja huo unataka maboresho ya ongezeko la asilimia 35, ambalo wanasema linahitajika ili kukabiliana na mfumuko mkubwa sana wa gharama za maisha uliojitokeza kwa miaka kadhaa.
Madaktari wadogo ni wenye ujuzi, mara nyingi wa miaka kadhaa, ambao wanafanya kazi kulingana za muongozo wa madaktari waandamizi na wao ni idadi kubwa ya jamii katika jumuiya ya matibabu.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.
Forum