“Ni lazima sote tufanye juhudi kuelekea sitisho la kudumu la mapigano, litakalopelekea Amani ya kudumu,” wanadiplomasia hao wamesema, wakiongeza kwamba hilo linahitaji kufanyika haraka iwezekanavyo.
Shirika la Afya Duniani, WHO, katika taarifa ya Jumapili limesema kwamba wafanyakazi wake wameshiriki kwenye zoezi la Umoja wa Mataifa la kutoa huduma za afya kwenye hospitali ya Shifa kaskazini mwa Gaza Jumamosi, wakipeleka dawa pamoja na vifaa vya upasuaji.
WHO imesema kwamba utendakazi wa hospitali hiyo umeathiriwa pakubwa wakati ikiwa na madaktari wachache tu pamoja na wauguzi, na takriban wafanyakazi 70 wa kujitolea. Ripoti zimeongeza kusema kwamba maelfu ya watu waliokimbia makwao wamechukua hifadhi ndani na nje ya jengo la hospitali hiyo.
Forum