Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:58

Washirika wa ulaya na Marekani wanalani Iran kuongeza kiwango cha uranium


Eneo jipya la chini ya ardhi la kiwanda cha nyuklia nchini Iran.
Eneo jipya la chini ya ardhi la kiwanda cha nyuklia nchini Iran.

Taarifa ya pamoja ya washirika inasema uzalishaji wa madini ya uranium yenye kiwango cha juu unaofanywa na Iran hauaminiki kuwa ni kwa malengo ya kiraia

Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na Marekani zimelaani suala la Iran kuongeza kiwango cha uzalishaji uranium yenye ubora wa hadi asilimia 60 karibu na kiwango kinachotumika kwa ajili ya matumizi ya silaha za nyuklia.

Katika taarifa ya pamoja washirika hao hawakutaja madhara yeyote ambayo Iran inaweza kukabiliana nayo kwa kuongezeka uzalishaji lakini wametoa wito kubadili hatua hiyo na kusema kuwa bado “wana nia ya dhati kwa suluhisho la kidiplomasia” kwa mzozo juu ya mpango wa nyuklia wa Tehran.

“Uzalishaji wa madini ya uranium yenye kiwango cha juu unaofanywa na Iran hauaminiki kuwa ni kwa maelngo ya kiraia”, ilisema taarifa hiyo. “mamuzi haya, yanawakilisha tabia ya kizembe katika muktadha wa kikanda ulio na mvutano”.

Tangu kuanza kwa mashambulizi ya Israel dhidi ya wanamgambo wa Hamas wanaotawala Gaza, washirika wanaoungwa mkono na Iran wameongeza mashambulizi yao katika meli kwenye Bahari ya Sham na kwa wanajeshi wa Marekani nchini Iraq na Syria, na kuongeza mvutano katika eneo hilo.

Israel ilianzisha operesheni yake katika kujibu mashambulizi yaliyosababisha vifo ya Hamas ya Oktoba 7 dhidi ya Israel.

Forum

XS
SM
MD
LG