Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:32

Waziri Mkuu wa Uingereza atafuta kura Bungeni kufanikisha mpango wa kuwapeleka waomba hifadhi Rwanda


Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak akiwa katika baraza kuu la bunge la Uingereza December 6, 2023. Picha na UK Parliament/Jessica Taylor/REUTERS
Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak akiwa katika baraza kuu la bunge la Uingereza December 6, 2023. Picha na UK Parliament/Jessica Taylor/REUTERS

Waziri Mkuu wa Uingereza alikuwa anahangaika siku ya Jumatatu kutafuta kura za kutosha kwa ajili ya sera yake uhamiaji ya kuwapeleka wanaoomba hifadhi nchini Rwanda baada ya wabunge wa chama chake kusema mpango wa sheria ya dharura hauna nguvu ya kutosha

Sunak anakabiliwa na mtihani muhimu kwa utawala wake, wakati wanasiasa wa mrengo wa kulia na kushoto wa chama cha Conservative wakitishia kuupinga mswaada huo hiyo wakati utakapofikishwa bungeni siku ya Jumanne.

Mwezi uliopita, mahakama ya juu ya Uingereza ilitangaza kuwa mpango wa serikali wa kuwapeleka maelfu ya wahamiaji nchini Rwanda ni kinyume cha sheria, ikisema kuwa taifa hilo la Afrika Mashariki halichukuliwi kama ni nchi ya tatu salama.

Akijibu, Sunak alikubali mpango mpya na Rwanda na alipitisha sheria mpya ya dharura yenye madhumini ya kubatilisha sheria ya ndani na ya kimataifa ya haki za binadamu ambazo zinaweza kuzuia kupelekwa kwa wahamiaji hao.

Hata hivyo kundi moja la wabunge limesema kuwa sheria hiyo haikwenda mbali vya kutosha katika kudhibiti rufaa kutoka kwa waomba hifadhi na kwamba inatoa tu “ sehemu na haitoi suluhisho kamili” wakisititiza tishio hilo kwa waziri mkuu.

Wabunge wamesema mswaada huo haufanya vya kutosha kuwazuia wahamiaji kuwasilisha madai yao wakidai kuwa Rwanda siyo nchi salama, na wala haiizuii makahama ya Ulaya ya Haki za Binaadamu kutiongilia kati.

Inahitaji wabunge wapatao 30 wa chama cha Conservative kupiga kura na chama cha upinzani siku ya Jumanne kuishinda sheria hiyo.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG