Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 08:55

Somalia yakubaliwa rasmi kuwa mwanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki


Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud akiwa na Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye.
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud akiwa na Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye.

Somalia imekubaliwa rasmi kuwa mwanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki huku Jumuia hiyo yenye nchi wanachama wanane sasa ikitafuta kupanua biashara huria katika kanda hiyo.

“Tumeamua kuikubalia Jamhuri ya shirikisho la Somalia chini ya mkataba wa kujiunga na Jumuia,” mwenyekiti wa Jumuia hiyo anayemaliza muhula wake, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amesema katika mkutano wa Jumuia hiyo mjini Arusha, Tanzania.

Somalia ambayo Rais wake Hassan Sheikh Mohamud alikuwa kwenye mkutano, inaungana na Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda.

Jumuia ya Afrika Mashariki yenye makao yake makuu mjini Arusha ambako mkutano huo ulikuwa unafanyika, ilianzishwa mwaka 2000, na inahusika na kuhimiza biashara kwa kuondoa ushuru wa forodha baina ya nchi wanachama.

Ilianzisha soko la pamoja mwaka wa 2010.

Forum

XS
SM
MD
LG