Bucyibaruta, ambaye alifariki Jumatano akiwa na umri wa miaka 79, alikuwa Mnyarwanda wa cheo cha juu zaidi aliyekabiliwa na kesi nchini Ufaransa kutokana na mauaji ya mwaka 1994 ambapo takriban Watutsi, 800,000 na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuwawa katika siku 100 za mauaji ya kimbari.
Bucyibaruta alipatikana na hatia Julai 2022, ya kushiriki mauaji na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika mkoa wa kusini wa Gikongoro, na kuhukumiwa kifungo cha miaka 20.
Akiwa mmoja wa Wanyarwanda wachache waliofikishwa mahakamani nchini Ufaransa, alikata rufaa dhidi ya hukumu hiyo na kuachiliwa kutoka gerezani akisubiri kesi mpya mpaka umauti ulipomkuta.
Forum