Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:40

Sunak awataka wabunge wa chama chake kuunga mkono mpango wake wa Rwanda


Waziri mkuu wa Uingereza akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Downing Street. Picha na James Manning/Pool via REUTERS
Waziri mkuu wa Uingereza akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Downing Street. Picha na James Manning/Pool via REUTERS

Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amewataka wabunge wa chama chake cha Conservative siku ya Alhamisi kuunga mkono mpango wake wa kuwapeleka Rwanda waomba hifadhi baada ya mpango huo kukataliwa na kubainisha migawanyiko mikubwa ndani ya chama chake.

Sunak anakabiliwa na changamoto kubwa sana katika kipindi chake cha mwaka mmoja madarakani wakati akijaribu kuwazuia wabunge wa chama hicho wa mrengo wa kulia wasipinge matakwa yao ya kuitaka Uingereza kuachana na mikataba ya kimataifa na kuwa na sera yake yenyewe ya uhamiaji.

Waziri wake wa uhamiaji alijiuzulu siku ya Jumatano na Sunak anakabiliwa na maswali kama anaweza kufanikisha sera yake kuu kupitia kura itakayopigwa katika bunge.

Baadhi ya wabunge wa Conservative wamesema siku ya Alhamisi kuwa Sunak anaweza kukabiliwa na changamoto za uongozi ndani ya chama ambacho kiko nyuma sana katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Katika mkutano na waandishi wa habari huko Downing Street, Sunak amesema kuwa bunge limeridhika na karibu kila ukosoaji uliotoka kwa wabunge wenzao, lakini iwapo serikali itaendelea zaidi kutofuata sheria za haki za binadamu, Rwanda itaachana na makubaliano hayo.

“Ni njia pekee kwa sababu tukiendelea zaidi, tofauti hiyo ni ya inchi moja, lakini ikiendelea zaidi maana yake kuwa Rwanda itaachana na mpango huo na kwamba hatutakuwa na sehemu nyingine ya kumpeleka mtu yeyote” alisema. “kitu ambacho kila moja anatakiwa afanye ni kuuunga mkono mswaada huu”

Rasimu ya sheria imekuja siku tatu baada ya maamuzi ya mahakama ya juu ya Uingereza kuwa Rwanda si mahali salama kuwapeleka wahamiaji wanaowasili kwa boti eneo la pwani lililoko Kusini mwa Uingereza, na mpango huo utakwenda kinyume na sheria ya kimataifa.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG