Hakuna maelezo yaliyotolewa kuhuisana na malengo ambayo yalipigwa, wala hakuna ripoti zozote za haraka za vifo. Shirika la habari la AFP limewakariri maafisa wa jeshi la anga wakisema kuwa shambulizi la Russia limetua aina mbali mbali ya silaha, zikiwemo, makombora ya masafa marefu, balistiki, na ndege zisizokuwa na rubani.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelsnskyy, katika hotuba yake ya kila siku kwa taifa Ijumaa amesema kwamba Januari 12 ni siku ambayo tayari imeingia kwenye historia ya taifa lake kwa kuwa Ukraine tayari imefikia makubaliano ya usalama na Uingereza, ambayo yamekuwa yakifanyiwa kazi kwa muda mrefu.
Waziri mkuu wa Uingerza Rishi Sunak aliitembelea Kyiv Ijumaa ili kuzindua ufadhili mpya wa kijeshi wa karibu dola bilioni 3.2 kwa Ukraine, ikiwa ni msaada mkubwa sana wa taifa hilo tangu Russia iivamie Ukraine.
Sunak alisema kwamba anatuma ujumbe kwa Ukraine kwa niaba ya taifa lake pamoja na washirika wa Ukraine kote duniani, kwamba kamwe hawataiacha peke yake. Amesema vita nchini Ukraine ni kuhusu haki yataif ahilo kujitetea lenyewe na kuwa demokrasia huru.
Forum