Somalia yamuamuru balozi wa Kenya kuondoka nchini

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo

Serikali ya Somalia imemuamuru balozi wa Kenya Mohamud Ahmed Nur Tarzan kuondoka nchini ikiishutumu Kenya kuiingilia kati masuala yake ya kisiasa.

Somalia pia imemtaka balozi wa Kenya nchini humo Lucas Tumbo kuondoka kwa ajili ya mashauriano.

Taarifa zinasema Somalia inaishutumu serikali ya Jubbaland kwa kukataa makubaliano ya uchaguzi yaliofikiwa septemba 17 katika uchaguzi utakaofanyika mwezi ujao.

Katibu Mkuu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia Mohamed Ali Nur amesema serikali imechukuwa uamuzi huu kulinda utaifa wake baada ya kuonekana kwamba kwa makusudi Kenya inaingilia masuala ya Somalia hasa Jubbaland.

Kenya inaunga mkono utawala wa Ahmed Mohamed Islam anaejulikana zaidi kama Madobe huko Jubbaland kwa sababu ya usalama wa Kenya na maslahi yake ya kikanda.

Kenya ina wanajeshi wake chini ya ujumbe wa Umoja wa Afrika nchini Somalia pamoja na Ethiopia .