Shambulizi la Uholanzi : Tanis achunguzwa kwa tukio la kigaidi

Gokmen Tanis

Waendesha mashtaka nchini Uholanzi wamesema Alhamisi watamfungulia mashtaka kadhaa yenye kusudio la kigaidi mshukiwa aliyefanya shambulizi la kinyama katika Jiji la Utrecht

Waendesha mashtaka wanaamini mzaliwa wa Uturuki Gokmen Tanis alitenda kosa hilo peke yake Jumatatu ambapo alidai kuwa amewaua watu watatu na kuwajeruhi wengine watatu.

Waendesha mashtaka na polisi wamesema katika tamko lao bado wanafanya uchunguzi iwapo mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 37 alitenda jinai hiyo ya kigaidi kwa kusudio lake binafsi au kutokana na matatizo yake binafsi yaliyokuwa yamechanganyika na fikra za msimamo mkali.

Mshukiwa huyo alikamatwa baada ya polisi kutumia saa nane kumfuatilia, hatua iliokaribia kusimamisha harakati zote jijini hapo. Baadae polisi walimkamata mshukiwa wa nne na wanajaribu kuchunguza iwapo mshukiwa huyu alihusika kutenda lolote kusaidia katika shambulizi hilo la silaha.”

Tanis amepangiwa kuhudhuria usikilizwaji wa kesi hiyo itakayofanyika faragha Ijumaa. Waendesha mashtaka pia wamesema Tanis atafanyiwa uchunguzi wa kisaikolojia.