Afisa mmoja wa ushirika huo amesema Jumatatu kwamba wanaunga mkono kwa dhati utaratibu wa kisiasa unaopendekezwa na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa (UN).
Siku ya Alhamisi iliyopita mungano huo unaongozwa na Saudi Arabia ulianzisha mashambulizi ya anga na ya nchi kavu katika lengo la kuuteka mji wa Hodeida kwenye bahari ya sham unaodhibitiwa na wapiganaji wa Kihouthi.
Mashambulizi yalikuwa yamesitishwa kabla ya kuanza mazungumzo ya amani mjini Geneva ambayo yalivunjika mwezi Septemba 2018.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths anasema hivi sasa ana matumaini ya kupanga mazunguimzo kati ya serikali na wahouthi mwezi huu.
Mapigano ya mwishoni mwa wiki yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 60 na dazeni kadhaa kujeruhiwa mjini Hodeida.