Sanamu la Bustani ya Tiananmen laondolewa Chuo Kikuu cha Hong Kong

Sanamu maarufu katika chuo kikuu cha Hong Kong, inayoonyesha kumbukumbu ya mauaji ya halaiki ya watu katika bustani ya Tiananmen ambayo imepangwa kuondolewa Chuo Kikuu cha Hong Kong (HKU) in Hong Kong, China October 12, 2021. REUTERS/Tyrone Siu

Sanamu maarufu katika chuo kikuu cha Hong Kong, inayoonyesha kumbukumbu ya mauaji ya halaiki ya watu katika bustani ya Tiananmen, imeondolewa Jumatano jioni.

Sanamu hiyo ilikuwa inaonyesha namna mauaji hayo yalivyokuwa, kwa kuonyesha miili ya watu ilivyorundikwa pamoja, kuonyesha maelfu ya wanaharakati wa kutetea demokrasia waliuawa na maafisa wa China mwaka 1989.

Ilikuwa mojawapo ya kumbukumbu pekee za umma Hong Kong, kuhusu mauaji hayo.

Hatua ya kuiondoa sanamu imetokea wakati Beijing imekuwa ukifanya msako mkali dhidi ya wapinzani wa kisiasa huko Hong Kong.

Mji wa Hong Kong ulikuwa miongoni mwa miji michache ambayo iliruhusu raia kuandaa maadhimisho ya maandamano ya bustani ya Tiananmen, ambapo ni swala nyeti sana nchini humo.

Mnamo mwaka 1989, maelfu ya watu walikusanyika katika bustan ya Tiananmen mjini Beijing, kudai uhuru wa kisiasa lakini baada ya wiki kadhaa, Juni tarehe 3, jeshi lilivamia sehemu hiyo na kuwapiga risasi waandamanaji kadhaa.