Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 00:10

Marekani, China watoa maonyo makali kabla ya mkutano wa Biden -Xi


FILE - Rais Joe Biden na Rais Xi Jinping in Brasília, Brazil, Nov. 13, 2019.
FILE - Rais Joe Biden na Rais Xi Jinping in Brasília, Brazil, Nov. 13, 2019.

Wanadiplomasia wa ngazi ya juu kutoka Marekani na China wametoa maonyo makali kuhusu suala nyeti la Taiwan, kabla ya mkutano mzito wa Jumatatu unaosubiriwa kufanyika kati ya viongozi wao.

Mkutano huo wa njia ya mtandao wa marais Joe Biden and Xi Jinping umekuja wakati mivutano inaendelea kuongezeka – kwa upande mmoja ikiwa juu ya Taiwan, demokrasia inayojiendesha yenyewe inayodaiwa na Beijing, lakini pia juu ya biashara, haki za binadamu na masuala mengine.

Katika mazungumzo ya simu Ijumaa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi wakijadili matayarisho ya mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ameeleza wasiwasi wake juu shinikizo la kijeshi, kidiplomasia na kiuchumi la Beijing dhidi ya Taiwan.

Wang alionya juu ya hatari kwa hatua za Marekani ambazo zinaweza kuonekana kama zinaunga mkono “uhuru wa Taiwan.”

Washington ilibadilisha msimamo wa kidiplomasia wa kuitambua Beijing na siyo Taipei mwaka 1979, lakini sheria iliyopitishwa na Bunge mwaka huohuo inaitaka Marekani kuwapa silaha Taiwan kwa ajili ya kujihami.

Serikali ya Marekani inatahadhari kutoonyesha wazi kuwa inaitambua Taiwan lakini inapata ushirikiano mpana wa pande zote mbili za kisiasa za Bunge la Marekani, wakati kikundi cha wabunge wakitembelea kisiwa hicho mwezi huu – Beijing ikikereka.

China imezidisha harakati za kijeshi karibu na Taiwan katika miaka ya karibuni, na kukiwa na rekodi ya idadi ya ndege zinazoingia katika eneo linalotambuliwa la ulinzi wa anga ya kisiwa hicho mapema Oktoba.

Washington imerejea kuonyesha uungaji mkono wake kwa Taiwan wakati imekuwa ikielezea juu ya uchokozi wa China.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la Habari la AFP

XS
SM
MD
LG