Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 03:33

Viongozi wa G20 wakutana mjini Roma kujadili masuala muhimu kimataifa


Wahudumu wa Afya waungana kwenye jukwaa na viongozi wa G20 katika kituo cha mkutano cha La Nuvola, mjini Roma, Italia, ili kupigwa picha ya pamoja.
Wahudumu wa Afya waungana kwenye jukwaa na viongozi wa G20 katika kituo cha mkutano cha La Nuvola, mjini Roma, Italia, ili kupigwa picha ya pamoja.

Mkutano mkuu wa G-20 ulioandaliwa na Italia ulianza Jumamosi mjini Roma, ambako viongozi kutoka nchi zenye uchumi mkubwa ulimwenguni, walijadili masuala mbalimbali muhimu, yakiwa ni pamoja na mikakati madhubuti ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, na janga la Corona.

Zulia jekundu lilizinduliwa kwa heshima ya viongozi hao katika kituo cha mikutano cha La Nuvola, wakati Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi, akimkaribisha Rais wa Marekani Joe Biden na viongozi wengine, huku masharti makali ya Covid-19 yakizingatiwa.

Mkutano huu ni wa kwanza kwa viongozi hao kuonana ana kwa ana katika kipindi cha miaka miwili, na unafuatia mkutano mkuu wa mwaka jana ulioandaliwa na Saudi Arabia.

Viongozi wa Rwanda na DCR pia walialikwa kwa mkutano huo kama waangalizi.

Wale hawakuhudhuria moja kwa moja na marais Vladmir Putin wa Russia, Xi Jinping wa China, na yule wa Mexico, Andrés Manuel López Obrador, ambao walijiunga nao kwa njia ya mtandao, kwa kile kinachoelezwa kuwa ni wasiwasi wa janga la Corona katika nchi zao.

Siku ya Ijumaa, mawaziri wa afya na fedha wa G-20 walitoa taarifa iliyoelezea kujitolea kwa nchi zao kudhibiti janga la Corona kote duniani kwa haraka iwezekanavyo.

Walisema G-20 itachukua hatua zote zinazohitajika ili kuendeleza malengo ya kimataifa ya chanjo ya angalau asili mia 40 ya idadi ya watu katika nchi zote za dunia mwishoni mwa mwaka huu, na asili mia 70 ifikapo katikati ya mwaka ujao, kama ilivyopendekezwa na Shirika la Afya Duniani. .

Hata hivyo, mawaziri hao hawakuweza kufikia makubaliano kuhusu utaratibu wa ufadhili na uratibu.

"Tunatafuta suluhisho la mwisho kwa mfumo wa ufadhili au matokeo ya mwisho ya jopo kazi au bodi ambayo itafanya kazi kama chombo cha kimataifa cha kuratibu," mshauri wa usalama wa kitaifa wa Marekani, Jake Sullivan, aliiambia VOA.

Mabadiliko ya tabianchi

Mjini Roma, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliuita mkutano huo kuwa ni fursa ya "kuweka mambo sawa" kabla ya mkutano wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa wa COP26 mjini Glasgow utakaoanza Jumatatu wiki ijayo, na ambao viongozi wa G-20 watashiriki kufuatia mkutano wao wa Italia.

XS
SM
MD
LG