Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 23:53

Mkutano wa China - Afrika watoa wito wa kuimarisha ushirikiano


Rais Xi Jinping wa China akihudhuria mkutano wa Africa - China mwaka 2019.Lintao Zhang/Pool via REUTERS
Rais Xi Jinping wa China akihudhuria mkutano wa Africa - China mwaka 2019.Lintao Zhang/Pool via REUTERS

Mkutano wa nane kati ya Afrika na China umefunguliwa rasmi Jumatatu mjini Dakar, mji mkuu wa Senegal, kukiwa na wito wa kuimarisha zaidi ushirikiano utakaoleta faida sawa kwa pande zote mbili. 

Viongozi wa mataifa hayo hawahudhuri mkutano huo kama ilivyo kawaida unapofanyika kila miaka mitatu badala yake ni kwa njia ya mtandao, hata hivyo Rais Xi Jingping atahutubia kwa njia ya vídeo mkutano huo wa siku mbili.

Masuala muhimu kwenye mazungumzo hayo ya ushirikiano kati ya Africa na China, FOCAC, ni biashara na usalama.

Wang Yi Feb.17, 2017. (Brendan Smialowski/Pool Photo via AP)
Wang Yi Feb.17, 2017. (Brendan Smialowski/Pool Photo via AP)

Katika mazungumzo yaliyofanyika jana kabla ya ufunguzi leo, mwenyeji wa mkutano waziri wa mambo ya nje wa Senegal Aissata Tall Sall amemuomba waziri mwenzake wa China Wang Yi kuiomba Bejing kujihusisha zaidi katika tatizo la ugaidi linaloongezeka hasa katika kanda ya Sahel huko Afrika Magharibi.

“Kwenye ushirikiano wetu na nchi za Sahel tungependa kuona ushawishi wa China unaongezeka na kuwa na nguvu zaidi, katika kuisaidia Senegal na nchi zote zinazokumbwa na tatizo la ukosefu wa usalama katika Sahel. Wanajeshi wetu wanapambana vikali na makundi ya kigaidi na ni matarajio yetu China itaungana nasi.”

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Tanzania Liberata Mulamula, akizungumza kabla ya mkutano amesema China ni rafiki wa muda mrefu wa Afrika na matarajio makubwa ni kuisaidia Tanzania kugeuka kuwa taifa la viwanda na kufikia malengo ya maendeleo endelevu.

Waziri Liberata Mulamula
Waziri Liberata Mulamula

Liberata Mulamula, “Utakuta kwamba asilimia 30 ya wafanyakazi wanategemea kilimo. Tukiweza kuimarisha sekta ya kilimo kuwa sekta ya viwanda vya uzalishaji bidhaa za kilimo, hivyo kuzipatia thamani bidhaa zetu jambo litakalotufikisha katika taifa la viwanda.”

China inajaribu kuimarisha ushirikiano wake wa nchi na nchi na kabla ya mkutano waziri wake wa mambo ya nje wang alikutana na mawaziri wa Sierra Leone, Zimbabwe na Msumbiji na kujadili namna ya kuwekeza zaidi katika nchi hizo.

Jana Eritrea na Guinea zimekuwa nchi mpya za Afrika kujiunga na mradi mkubwa wa China barabara ya sufi, BRI, na kufikisha idadi ya nchi za Afrika kujiunga na mradi huo kuwa 48.

Wakazi wa Dakar wakizungumza leo wamepongeza ushirikiano na msaada mkubwa unaotolewa na China kwa nchi za Afrika lakini wangelipenda kuona uhusiano mkubwa zaidi katika afya na technolojia. Papis Coly ni mchambuzi wa uhuisano kati ya Afrika na China mjini Dakar.

Coly amesema : “Uwanja wa michezo wa urafiki, kituo cha maendeleo cha Diamniadio na miradi mingine mingi na matunda ya ushirikiano mzuri kati ya China na Senegal. Lakini matumaini yetu ni kwamba kupitia ushirikiano huu ingelibidi china kusiadia Senegal kujenga vituo vya afya.”

Kwenye mkutano huu mawaziri watatathmini mafanikio yaliyopatikana kufuatia mazungumzo ya Bejing ya viongozi wa juu ya vita dhidi ya janga la Corona. Na wakati huo huo watazungumza juu ya ajenda ya maendeleo na ushirikiano kati ya pande mbili mnamo miaka mitatu ijayo.


XS
SM
MD
LG