Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 07:20

G20: Viongozi wakubaliana kuhusu mkakati wa kupunguza viwango vya joto duniani


Baadhi ya viongozi wa nchi wanachama wa G-20 wakati wa mkutano mkuu katika kituo cha La Nuvola mjini Roma, Italia, Okt. 31, 2021. (Aaron Chown/Pool Picha ilipigwa na AP)
Baadhi ya viongozi wa nchi wanachama wa G-20 wakati wa mkutano mkuu katika kituo cha La Nuvola mjini Roma, Italia, Okt. 31, 2021. (Aaron Chown/Pool Picha ilipigwa na AP)

Jumapili ilikuwa siku ya pili na ya mwisho ya mkutano mkuu wa nchi zenye uchumi mkubwa zaidi duniani, G-20, mjini Roma, Italia, ambako, kati ya mengine, viongozi wa mataifa hayo wanajadili mikakati ya kukabiliana na tishio lililopo la mabadiliko ya hali ya hewa licha ya baadhi ya wadau wakuu kutohudhuria ana kwa ana.

Hayo yaliendelea kabla ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa, COP26, mjini Glasgow, Scotland, kuanzia Jumapili Oktoba 31.

Katika maazimio yao, viongozi waliahidi kuchukua hatua za haraka ili kufikia lengo la kupunguza ongezeko la joto duniani hadi nyuzi joto 1.5, kulingana na ahadi ya kimataifa iliyotolewa mwaka 2015, katika Mkataba wa Paris wa hali ya hewa wa kuweka joto duniani kuwa "chini ya nyuzi 2 za Celsius, zaidi ya viwango vya kipindi cha kabla ya viwanda kuanza kuchafua mazingira, na ikiwezekana, hadi digrii 1.5 Celcius.

Kundi la nchi 19 na Umoja wa Ulaya, linachangia zaidi ya robo tatu ya uzalishaji wa gesi chafuzi duniani. Nchi hizo zilihitajika kupata makubaliano juu ya kufikia upunguzaji wa hewa chafu, haswa juu ya kupunguza uzalishaji wa gesi ya methane, na kusitisha matumizi wa makaa ya mawe.

Nchi kumi na mbili mwezi huu zimejiunga na juhudi zinazoongozwa na Marekani na Umoja wa Ulaya kupunguza uzalishaji wa methane kwa asili mia 30, ifikapo 2030.

Hata hivyo, viongozi wa nchi kama vile China na Russia, ambazo ni kati ya wachafuzi wakuu wa mazingira duniani, hawatahudhuria mkutano wa COP 26 ana kwa ana na wala hawakuhudhuria ule wa G20.

XS
SM
MD
LG