Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema Jumanne kwamba Marekani itafanya kazi na washirika kutetea na kuhamasisha uhuru na uwazi katika eneo la Indo-Pacific.
Akizungumza wakati wa ziara yake nchini Indonesia, Blinken alisema nguvu kubwa zaidi dhidi ya vitisho vinavyoendelea ni kufanya kazi na mataifa mengine, na kwamba Marekani inataka kuhakikisha watu na nchi zina uhuru wa kuamua juu ya mustakabali wao wenyewe na washirika.
Tutapitisha mkakati ambao unaunganisha kwa karibu zaidi vyombo vyetu vyote vya nguvu ya kitaifa, diplomasia, kijeshi, kijasusi na washirika wetu alisema.
Blinken alisisitiza kujitolea kwa Marekani kwa uhuru wa usafiri katika Bahari ya Kusini ya China, eneo ambalo alisema hatua za China zinatishia usafirishaji wa bidhaa za dola trilioni 3 kila mwaka.