Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ni miongoni mwa viongozi wachache wanaohudhuria mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York ambao kwa sehemu kubwa unafanyika kwa njia ya mtandao.
Karibu viongozi 100 watahudhuria mkutano huo kupitia mtandao baada ya kushauriwa kutokwenda New York katika juhudi za kupambana na janga la COVID-19.
Akizungumza na Idhaa wa Kiswahili alipowasili New York hapo Jumapili Rais Samia alisema atahudhuria vikao mbali mbali lakini anatilia mkazo zaidi suala la Mabadiliko ya hali ya hewa na jinsi nchi yake inavyokabiliana na janga hilo.
Bi Samia ambaye atauhutubia mkutano wa Baraza Kuu siku ya Alhamisi amesema mbali na kuhudhuria mazungumzo juu ya masuala mbali mbali ya Umoja wa Mataifa amefuatana na ujumbe muhimu wa wafanyabiashara kwa ajili ya kukutana na wafanyabiashara wa Marekani.