Rais Biden atarajiwa kukutana na Waziri Mkuu Johnson

Rais Joe Biden akiongea na wajumbe wa Marekani huko RAF Mildenhall, Suffolk, Uingereza, Juni 9, 2021, baada ya kuwasili Ulaya ili kukutana na washirika wa Marekani na Rais wa Russia Vladimir

Rais wa Marekani Joe Biden atakutana Alhamisi na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson kwenye safari yake ya Ulaya.

Ziara yake Biden inajumuisha mazungumzo ya kiwango cha juu na wakuu wengine wa nchi za Magharibi na mkutano na Rais wa Russia Vladimir Putin.

Ulimwengu utakuwa ukiangalia jinsi Biden na Johnson watakavyoshirikiana baada ya kutokubaliana hapo awali juu ya sera, pamoja na Brexit.

Juu ya Brexit utawala wa Obama na Biden ulipinga uamuzi wa Uingereza kuhama Umoja wa Ulaya (EU).

Kemia haikuwa nzuri kwani Rais Biden alikuwa amemwita Boris Johnson kama mfano wa Donald Trump, alisema Dan Hamilton, mkurugenzi wa Global Europe Program katika Kituo cha Wilson nchini Marekani.

Chanzo cha Habari : VOA NEWS