Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:16

Biden azitaka taasisi 6 kupendekeza wahamiaji gani waruhusiwe kubakia


Rais Joe Biden
Rais Joe Biden

Utawala wa Rais wa Marekani Joe Biden imetwika jukumu kwa makundi 6 ya kibinadamu kupendekeza ni aina gani ya wahamiaji wanaoweza kuruhusiwa kubaki hapa Marekani.

Fursa hiyo itakuwa kinyume na utaratibu uliokuwepo wa wahamiaji kurejeshwa makwao mara moja chini ya kanuni maalum za wakati huu wa janga la corona, zinazozuia watu kuomba hifadhi.

Makundi hayo sasa yataamua ni nani anayehitaji kupewa hifadhi kutoka Mexico japo mikakati hiyo haijawekwa wazi kwa umma.

Hatua hiyo inakuja wakati kukiwa na wimbi kubwa la watu wanaoomba hifadhi kwenye mpaka wa kusini wa Marekani.

Pia serikali imeombwa kuondoa kanuni zilizowekwa wakati wa utawala wa Trump na kuendelezwa wakati wa Biden, za kutoruhusu wahamiaji ndani ya nchi wakati huu wa janga la corona.

Kufikia sasa karibu wahamiaji 800 wameruhusiwa kuingia hapa Marekani tangu Mei 3 wakati makundi yaliotwikwa jukumu la kutathmini wanaoweza kuruhusiwa kuingia yakisema kuwa kuna idadi kubwa ya waomba hifadhi kushinda uwezo wao.

Kando na kamati ya kimataifa ya uokozi, hakuna makundi mengine yaliyo tajwa kwa umma kufikia sasa.

XS
SM
MD
LG