Rais anataka kusisitiza mapendekezo yake juu ya jinsi nishati safi itakavyosaidia kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa na kufungua nafasi za ajira zinazolipa.
"Mswaada wetu wa pande mbili wa miundombinu una uwekezaji mkubwa wa serikali kuu, usambazaji wa umeme katika historia yetu, ili gridi yetu iwe ya uhakika zaidi tunaweza kuwa na nishati mbadala zaidi, ili tuweze kufungua nafasi nzuri zaidi za ajira katika ujenzi wa gridi hiyo mpya," akiongeza,
"Pia tunafanya uwekezaji mkubwa katika usafiri wa umma, mabasi ya umeme. Huko Denver tutamsaidia Meya Hancock kufanikisha lengo lake la kupunguza gesi chafu kwa asilimia 80,” amesema Rais Biden
Ziara hiyo inatoa nafasi kwa Rais Biden kuendelea na mpango wake wa matumizi na kupambana na tishio la haraka linalosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
Rais Biden amesema kitu kilichosababishwa na mwanadamu kinaweza kubadilishwa na mwanadamau.