Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:43

Seneti ya Marekani yapitisha mswada wa miundombinu wa dola trilioni 1.2


Daraja inayoendelea kujengwa.
Daraja inayoendelea kujengwa.

Baraza la Seneti la Marekani Jumanne lilipitisha mswada wa kuboresha miundombinu wa dola trillioni 1.2 ambao utaboresha barabara na madaraja yaliyoharibika, na kupanua huduma ya mtandao wa internet wenye kasi ya juu nchini kote.

Mradi huo ulipitishwa kwa kura 69 dhidi ya 30, maseneta Warepublican 19 wakijiunga na Wademocrats 50 kuupigia kura, ikiwa moja ya juhudi kubwa za kuwekeza kwenye miundombinu hapa Marekani kwa kipindi cha miaka kadhaa. Mradi huo utawasilishwa kwenye baraza la wawakilishi ambalo litaanza kuujadili mwezi Septemba.

Ikulu ya Marekani inaunga mkono mradi huo, moja ya ahadi kubwa za rais Joe Biden wakati wa kampeni yake ya mwaka wa 2020.

Kando na kukarabati barabara na madaraja na kupanua mtandao wa internet, mradi huo utabadilisha mabomba ya kusafirisha maji ya kunywa, kupanua mfumo wa usafiri wa reli na kuboresha viwanja vya ndege.

Biden ambaye amewapongeza maseneta warepublican na Democrat kwa kufanya kazi pamoja, amesema mradi huo utaongeza ajira laki 2 kila mwaka katika mwongo mmoja ujao.

XS
SM
MD
LG