Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:13

Biden na maseneta kujadili makubaliano ya mradi wa miundombinu


Rais Joe Biden
Rais Joe Biden

Rais wa Marekani Joe Biden Alhamisi inatarajiwa kukutana huko White House na kundi la maseneta wa vyama vya Republican na Democrat baada ya maseneta hao kueleza kwamba wamepiga hatua ya kuridhisha kufikia makubaliano juu ya matumzi ya fedha kwenye mradi wa miundombinu wa Biden.

Mazungumzo ya hivi karibuni yalijikita kwenye mpango wa matumzi ya zaidi ya dola trillioni 1.

Malengo maalum ya mradi huo ni kuboresha barabara za kitaifa, mtandao wa umeme na kupanua upatikanaji wa mtandao wa internet nchini kote.

Awali, Rais Biden alipendekeza bajeti ya dola trillioni 2.3 baadaye akaipunguza hadi kwenye dola trillioni 1.7 ili kupata uungwaji mkono wa Warepublican kufanikisha mradi wake kwenye baraza la seneti lililogawanyika juu ya gharama ya mradi huo.

Moja ya suala lililosababisha mgawanyiko kati Warepublican na Wademocrat ni kuhusu namna ya kufadhili mradi huo.

Biden alipendekeza kuongeza kodi kwenye mapato ya makampuni, lakini wa Republican walipinga pendekezo hilo.

Chanzo cha Habari : VOA News

XS
SM
MD
LG