Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:59

Udukuzi : Kampuni ya Colonial Pipeline yaanza kusafirisha mafuta vituoni


Kufuatia udukuzi wateja wakinunua mafuta ya ziada kwa hofu ya Luweno upungufu wa mafuta hukoTampa, Florida,Marekani, Mei 12, 2021. REUTERS/Octavio Jones
Kufuatia udukuzi wateja wakinunua mafuta ya ziada kwa hofu ya Luweno upungufu wa mafuta hukoTampa, Florida,Marekani, Mei 12, 2021. REUTERS/Octavio Jones

Kampuni ya kusafirisha mafuta katika kanda ya mashariki ya Marekani, Colonial Pipeline, imetangaza Ijumaa imeanza kusafirisha kwa ukamilifu mafuta.

Usafirishaji huo umerejea kwa vituo vyote katika kanda hiyo baada ya upungufu wa wiki moja, kufuatia shambulio la udukuzi kwenye liliosababisha kuzimwa mitambo yake.

Shambulio hilo ambalo lilikuwa kubwa kabisa kutokea katika miundombinu ya nishati ya Marekani lilisababisha taharuki katika majimbo ya kusini mashariki ya Marekani ambapo bei ya mafuta ilipanda na waendesha magari kukimbilia kujaza mafuta kwenye magari yao.

Taharuki hiyo ilisababisha mlolongo wa magari katika vituo vya kujaza mafuta kwa wiki nzima.

Colonial Pipeline ilitangaza jana usiku kwamba mitambo yake imeanza kufanya kazi na hivyo usafirishaji mafuta kupitia mabomba yake mawili makuu yananaza kazi kwa ukamilifu leo.

Rais Joe Biden aliwahakikishia waendesha magari hapa Marekani kwamba utowaji mafuta unatarajiwa kurudi katika hali ya kawaida mwishoni mwa wiki hii.

XS
SM
MD
LG