Rais Biden hajazungumza hadharani tangu Jumapili, wakati rais huyo mwenye umri wa miaka 80 alipoiunga mkono kwa dhati Israeli, majibu yake kuhusu uwezekano wa mzozo wa mateka na tishio la vita vya kikanda linafuatiliwa kwa karibu sana.
Rais amesema kwamba Wamarekani kuwa huenda wakawa miongoni mwa wale waliotekwa na kupelekwa Gaza na kundi la wanamgambo wa Palestina Hamas katika shambulio la kushutukiza huko Israel siku ya Jumamosi, wakati takriban Wamarekani 11 wameuawa.
Biden na Makamu wa Rais Kamala Harris walitarajiwa kuzungumza na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu siku ya Jumanne asubuhi baada ya kukutana na timu zao za usalama wa taifa, White House ilisema.
Pamoja na Netanyahu "wangejadili uungaji mkono wetu kwa Israeli" na juhudi za "kuwazuia wengine wenye uhasama kutumia vibaya shambulio hili dhidi ya Israeli" – ikiimaanisha dhahiri Iran, ambayo inaiunga mkono Hamas, na kundi la wanamgambo la Hezbollah linaloendesha shughuli zake kutoka kusini mwa Lebanon.
Rais Biden anatarajiwa kuhutubia saa moja jioni kutoka White house.
Chanzo cha habari ni Shirika la habari la AFP