Mshauri wa usalama wa taifa wa Korea Kusini, Cho Tae-yong, anachunguza athari zinazoweza kusababishwa na mzozo wa Hamas, na Israel, kwa usalama wa Korea Kusini, ilisema ofisi ya Rais Yoon Suk Yeol, Jumatatu.
Shambulio la Hamas dhidi ya Israel, Jumamosi, ambalo ni baya zaidi kutokea katika kipindi cha miaka 50, lilionekana kuongeza mzozo na kuwa vita kamili kwa siku zake sasa.
Jeshi la Israel limewakusanya askari wa akiba 300,000 Jumatatu wakati likiendelea na mashambulizi ya kujibu ya mashambulizi ardhini, angani na baharini ya Hamas.
Israel pia imeweka kizuizi kamili cha Ukanda wa Gaza unaodhibitiwa na Wapalestina.
Forum