Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 17, 2024 Local time: 23:39

Shambulio lakipiga kivuko mpakani mwa Misri na Israel


Makombora yaliyorushwa kutoka Ukanda wa Gaza yakinaswa na mfumo wa makombora ya ulinzi ya Israel katika mji wa Ashkelon uliopo kusini mwa Israel Oktoba 10, 2023. Picha na JACK GUEZ / AFP.
Makombora yaliyorushwa kutoka Ukanda wa Gaza yakinaswa na mfumo wa makombora ya ulinzi ya Israel katika mji wa Ashkelon uliopo kusini mwa Israel Oktoba 10, 2023. Picha na JACK GUEZ / AFP.

Kivuko cha mpakani cha Rafah huko Gaza kilichopakana na Misri, ambacho ndiyo pekee cha kuingia Israel, kimepigwa na shambulio la anga la Israel siku ya Jumanne kwa mara ya pili katika kipindi cha ndani ya saa 24, mpiga picha wa shirika la habari la AFP ameripoti.

Walioshuhudia wamesema shambulio hilo liligonga ardhi ambayo haikaliwi na mtu, iliyoko kati ya milango ya Misri na Palestina, na kuharibu ukumbi wa upande wa Palestina.

Shirika la habari la AFP lilipowasiliana na, jeshi la Israel lilisema "haliwezi kuthibitisha au kukanusha" shambulio lolote lililotokea kwenye kivuko "wakati huu".

Kundi la Misri la Sinai kwa Haki za Binadamu limesema shambulio hilo lilisababisha kufungwa kwa kivuko hicho lakini hakuna uthibitisho uliopatikana kwa haraka kutoka pande zote mbili.

Ilikuwa ni mara ya pili kwa kivuko hicho kupigwa, tangu Israel ilipoanzisha mashambulia makali ya mabomu eneo la Gaza kujibu shambulizi la ghafla lililofanywa na watawala wa Hamas siku ya Jumamosi na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 900 nchini Israel.

Shambulio la awali la Jumatatu, lilisitisha kwa muda njia inayotumika katika kivuko hicho, chanzo cha usalama na mashahidi walisema.

Hakuna maoni yoyote kutoka mamlaka ya Misri.

Israel imetangaza "kuizingira kabisa" Gaza, kukata chakula, maji na usambazaji wa umeme kwa watu milioni 2.3 wa eneo hilo.

Chanzo cha habari ni Shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG