Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 17:37

Netanyahu: Israeli 'ndio imeanza' kujibu shambulizi lililofanywa na Hamas


Wapalestina wakikagua uharibifu uliofanywa na mashambulizi ya Israeli katika vita inayoendelea huko Gaza.
Wapalestina wakikagua uharibifu uliofanywa na mashambulizi ya Israeli katika vita inayoendelea huko Gaza.

Israel imesema Jumanne jeshi lake limeshambulia  mamia ya malengo huko ukanda wa Gaza usiku kucha, saa kadhaa baada ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kusema kuwa vikosi vyake vilikuwa ndiyo  vimeanza kuwashambulia wanamgambo wa Hamas.

Benjamin Netanyahu(Photo by Iakovos Hatzistavrou / POOL / AFP)
Benjamin Netanyahu(Photo by Iakovos Hatzistavrou / POOL / AFP)

Msemaji wa jeshi Richard Hecht amesema miili 1,500 ya wapiganaji wa Hamas imepatikana Israel kufuatia uvamizi wao wa jumamosi na kwamba hakuna wanamgambo wowote waliovuka kuingia Israel tangu jumatatu.

Mashambulizi ya anga yalilenga ujirani wa Rimal huko Gaza City ambako kuna wizara nyingi na majengo ya serikali ya hamas.

“ Tutakachokifanya kwa maadui zetu katika siku zijazo kitakumbukwa hadi vizazi vyao vijavyo,” Netanyahu alisema katika hotuba yake Jumatatu jioni.

Jeshi la Israel limesema linakusanya wanajeshi wa akiba laki tatu kabla ya kufanya mashambulizi ili kujibu uvamizi wa kushtukiza wa Hamas jumamosi katika maeneo ya Israel huko ukanda wa Gaza .

msemaji wa jeshi la Hamas amesema wapiganaji wake watauwa mmoja wa mateka 150 wanaowashikilia wakati wowote Israel itakapolenga maeneo ya kiraia huko Gaza bila onyo.

Waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant alisema katika taarifa ya Video kwamba Israel itaizingira gaza na kulikatia mawasliano eneo la palestina pmaoja na kukata umeme , chakula , maji na gesi.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres amewaambia waandishi wa habari kuwa anatambua uhalali wa wasiwasi wa usalama wa Israel, lakini operesheni za kijeshi lazima zifanyike kwa kufuata sheria za kibinadamu. Amesema raia lazima walindwe na miundo mbinu isilengwe.

Forum

XS
SM
MD
LG