Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 13:10

Israel inasema imefanya mashambulizi dhidi ya maeneo ya Hamas


Mapigano yanayoendelea kati ya wa-Palestina na Israel
Mapigano yanayoendelea kati ya wa-Palestina na Israel

Msemaji mwingine, Luteni Kanali Jonathan Conricus alisema Israel iliwaongeza wanajeshi 100,000 wa akiba.

Israel imesema Jumatatu ilifanya mamia ya mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo ya Hamas katika Ukanda wa Gaza, wakati vikosi vya Israel vikifanya kazi ya kuwaondoa wanamgambo wa Hamas ambao bado wanapigana kusini mwa Israel.

Msemaji wa jeshi la Israel, Luteni kanali Richard Hecht aliwaambia waandishi wa habari kwamba mapigano yalikuwa bado yakiendelea katika maeneo saba hadi nane huko Israel na kwamba ilichukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa kujibu uvamizi ulioanza Jumamosi.

Msemaji mwingine, Luteni Kanali Jonathan Conricus, alisema Israel iliwaongeza wanajeshi 100,000 wa akiba.

Kazi yetu ni kuhakikisha kwamba mwishoni mwa vita hivi Hamas haitakuwa tena na uwezo wowote wa kijeshi wa kuwatishia raia wa Israeli, Conricus alisema katika video iliyowekwa kwenye mtandao wa X. Pamoja na hayo, pia tutahakikisha kuwa Hamas haitaweza kutawala Ukanda wa Gaza.

Forum

XS
SM
MD
LG