Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 20:14

Wanafunzi wawili wakitanzania nchini Israel hawajulikani walipo


Moshi mkubwa ukiwa umetanda katika anga ya Mji wa Gaza wakati wa shambulizi la anga la Israel Oktoba 9, 2023. Picha na MAHMUD HAMS / AFP.
Moshi mkubwa ukiwa umetanda katika anga ya Mji wa Gaza wakati wa shambulizi la anga la Israel Oktoba 9, 2023. Picha na MAHMUD HAMS / AFP.

Watanzania wawili hawajulikani walipo wakati mapigano yakiendelea Kusini mwa Israeli kufuatia mashambulizi ya kushtukiza Jumamosi na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 1,200.

Akizungumza na Sauti ya Amerika, balozi wa Tanzania nchini Israel, Alex kalua amesema Watanzania hao ambao hawajulikani walipo ni miongoni mwa wanafunzi 260 waliokuwa wanachukua mafunzo ya kilimo katika vyuo mbalimbali vilivyopo katika eneo la Kusini ambalo limekumbwa na mashambulizi.

Hata hivyo balozi huyo hakuweza kutaja majina ya wanafunzi hao wala vyuo walivyokuwa wakisoma.

Amesema “Inawezekana kutokana na purukushani huenda wakawa wamepoteza simu, wako kwenye eneo ambalo wamejificha kwa hiyo hawana mawasiliano”

“Kuna uwezekano pengine baadhi wametekwa, kama unavyofahamu inasemekana kwamba zaidi ya watu 100 walitekwa na hilo kundi na wamepelekwa Gaza” aliongeza balozi huyo.

Balozi Kalua pia amesema mwanafunzi mwengine wa kitanzania aliyekuwa amepotea amepatikana, hakuweza kutaja jina la mwanafunzi huyo wala chuo alichokua akihudhuria, lakini amasema mamlaka zimemtumia taarifa na picha za mwanafunzi huyo ambaye aliyekuwa amejificha kwenye handaki.

Wanajeshi wa Israel wakiwa mpakani jirani na eneo la Gaza lililopo Kusini mwa Israel Oktoba 9, 2023. Picha na JACK GUEZ / AFP.
Wanajeshi wa Israel wakiwa mpakani jirani na eneo la Gaza lililopo Kusini mwa Israel Oktoba 9, 2023. Picha na JACK GUEZ / AFP.

Wakati huo huo Misri imeongeza msukumo wa juhudi za kidiplomasia siku ya Jumatatu kuzuia ghasia hizo kusambaa huko Gaza na Israel, ofisi ya rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri ilisema.

Rais al-Sisi, ambaye nchi yake kihistoria imekuwa mpatanishi mkuu kati ya Israel na Palestina, alizungumza na rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mohamed bin Zayed Al Nahyan, wakikubaliana "kuimarisha majadiliano na juhudi za kidiplomasia kusitisha kusambaa kwa harakati za kijeshi", alisema msemaji wa rais Sisi.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa Misri pia inahakikisha ulinzi wa Waisraeli waliochukuliwa mateka na wanamgambo wa Kipalestina, vyanzo viwili vya usalama vya Misri vilisema Jumatatu.

Misri iliisihi Israeli kujizuia na Hamas ambayo inawashikilia mateka kuwaweka katika hali nzuri ili kutoa nafasi ya uwezekano wa kupunguza mapigano haraka, ingawa mashambulizi mfululizo yanayofanywa na Israeli huko Ukanda wa Gaza yanafanya upatanishi huo kuwa mgumu, kilisema chanzo hizo kwa sharti la kutotajwa jina.

Baadhi ya taarifa ya habari hii inatoka mashirika ya habari ya Reauters na AFP

Forum

XS
SM
MD
LG