"Mamia ya magaidi" wameuawa na kukamatwa, afisa wa kijeshi wa Israeli alisema, kufuatia shambulio la kushtukiza la kundi la wanamgambo wa Kipalestina lenye makao yake katika Ukanda wa Gaza.
Jeshi la Israeli liliripoti mapigano katika maeneo kadhaa ya kusini, karibu na Ukanda wa Gaza ambapo kundi la Hamas lilianzisha mashambulizi yake Jumamosi. Maeneo hayo yalijumuisha jiji la Sderot.
Luteni Kanali Jonathan Conricus, msemaji wa IDF, aliambia shirika la habari la CNN kwamba huenda kulikuwa na wapiganaji 1,000 wa Hamas walioingia Israeli siku ya Jumamosi.
Wakati huo huo, Israeli inatafuta usaidizi kutoka Misri ili kuthibitisha habari kuhusu hali ya usalama wa raia wake iwaliotekwa nyara, na maeneo waliko, kulingana na ripoti katika gazeti la Wall Street Journal.
Hamas na jeshi la Israeli wamesema Hamas waliwachukua mateka wanajeshi wa Israeli na raia siku ya Jumamosi, lakini idadi kamili haijajulikana.
Israeli ilitekeleza mashambulizi zaidi ya kulipiza kisasi katika Ukanda wa Gaza siku ya Jumapili. IDF ilisema kuwa makao makuu ya kijasusi ya Hamas, kiwanda cha kutengeneza silaha na benki mbili ni miongoni mwa shabaha ambazo vikosi vyake vimefikia hadi sasa.
Hamas waliendelea na mashambulizi yake usiku kucha pia, wakirusha makombora katika miji kadhaa, ikiwa ni pamoja na Tel Aviv.
Mgogoro huo mbaya zaidi katika miongo kadhaa umesababisha vifo vya zaidi ya 600 upande wa Israel, ofisi ya vyombo vya habari vya serikali ilisema, huku maafisa wa Gaza wakiripoti vifo vya takriban 370, na maelfu zaidi kujeruhiwa kila upande.
Wizara ya Afya ya Palestina mjini Gaza imesema takriban watu 256 wamefariki katika mashambulizi hayo wakiwemo watoto 20 huku watoto 121 wakiwa miongoni mwa watu 1,788 waliojeruhiwa.
Marekani, mshirika wa karibu na msambazaji mkuu wa silaha kwa Israel, huenda ikatangaza msaada mpya wa kijeshi Jumapili kufuatia shambulio la Hamas, Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken alisema.
"Tunatathmini maombi ya ziada ambayo Waisraeli wametoa. Nadhani kuna uwezekano wa kusikia zaidi kuhusu hilo baadaye leo," Blinken aliliambia shirika la habari la CNN.
"Maelekezo ya Rais Joe Biden ni kuhakikisha kwamba tunaipatia Israeli kila kitu inachohitaji katika wakati huu ili kukabiliana na mashambulizi kutoka kwa Hamas."
"Tuna ripoti kwamba Wamarekani kadhaa waliuawa. Tunajaribu kuthibitisha hilo. Wakati huo huo, kuna ripoti za Wamarekani waliopotea, na tunajaribu kuthibitisha ripoti hizo," Blinken alisema.
Blinken baadaye Aliiambia shrika la habari la ABC kwamba "hili ni shambulio kubwa la kigaidi ambalo linawaua raia wa Israeli katika miji yao, majumbani mwao, na kama vile tumeona kwa uwazi, kuwaburuta watu kuvuka mpaka na Gaza.
Forum