Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 17:34

Israel yadai kuwa miili 1,500 ya wapiganaji wa Hamas imepatikana nchini humo


Baadhi ya majengo yaliyoharibiwa na mashambulizi ya Israel kwenye mji wa Gaza City. October 10, 2023.
Baadhi ya majengo yaliyoharibiwa na mashambulizi ya Israel kwenye mji wa Gaza City. October 10, 2023.

Israel imesema mapema Jumanne kwamba jeshi lake limeshambulia mamia ya malengo huko  Ukanda wa Gaza usiku kucha baada ya waziri mkuu  Benjamin Ntenyahu kusema kwamba majeshi ya nchi yake yalikuwa katika mwanzo wa mapambano dhidi ya wanamgambo wa Hamas.

Msemaji wa jeshi Richard Hecht amesema kwamba miili 1,500 ya wapiganaji wa Hamas imepatikana ndani ya eneo la Israel kufuatia uvamizi wa Jumamosi, na kwamba hakuna mwanamgambo aliyevuka na kuingia Israel tangu Jumatatu.

Miongoni mwa maeneo yaliyolengwa na Israel ni pamoja na ujirani wa Rimal ulioko Gaza City, ambao ni makazi ya wizara na majengo ya serikali ya Hamas. Katika hotuba yake Jumatatu, Ntenyahu alisema kwamba, “Kile watakachokifanya kwa adui wetu kitakumbukwa kwa vizazi vijavyo.”

Hamas kupitia msemaji wake ilisema kwamba wapiganaji wake wanaweza kuwaua mateka wa Israel 150 wanaowashikilia, mmoja baada ya mwingine kila wakati Israel inapowalenga raia bila kutoka tahadhari. Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant kupitia taarifa ya Jumatatu alisema kwamba Israel ingekatiza huduma zote muhimu kwa Gaza zikiwemo umeme, chakula, maji na gesi.

Forum

XS
SM
MD
LG