Nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara zinaathirika zaidi na ugaidi – Wataalamu

Wakazi wa eneo hilo wakiwa wamekusanyika nje ya Mgahawa wa Pearl Beach, baada ya kushambuliwa na wanamgambo wa Al Shabaab huko Mogadishu, terehe 10 Juni 2023. Picha na REUTERS/Feisal Omar.

Wataalamu wa masuala ya kukabiliana na ugaidi walisema Jumanne kwamba, kwa sasa Afrika ndiyo sehemu inayoathiriwa zaidi na ugaidi duniani.

Walisema nusu ya waathirika waliouawa mwaka jana ni kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara, ingawa washirika wa al-Qaida na Islamic State bado wameenea na kuendelea kufanya mashambulizi katika maeneo mengine duniani.

Interpol, shirika la kimataifa la polisi linaloshughulikia uhalifu, pia liliripoti katika jopo la majadiliano yaliyofanyika Umoja wa Mataifa, kwamba ugaidi unahusishwa na itikadi kali za mrengo wa kulia ziliongezeka kwa mara 50 katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, hususani huko Ulaya, Amerika Kaskazini na sehemu za Asia-Pacific.

Wataalamu wanaona mienendo mingine: Kudorora kwa usalama wa kimataifa kunasababisha tishio la ugaidi " mkanganyiko mkubwa zaidi na yaliyosambaa." Watu wenye msimamo mkali wanazidi kutumia teknolojia ya hali ya juu, na ndege zisizo na rubani na akili bandia ambazo zimefungua njia mpya za kupanga na kutekeleza mashambulizi.

Umoja wa Mataifa wiki hii unaandaa mkutano wake wa tatu wa ngazi ya juu wa wakuu wa mashirika ya kukabiliana na ugaidi. Jopo la Jumanne la kutathmini mienendo na vitisho vya ugaidi vinavyoibuka na vilivyoendelea ambavyo vimewafanya wataalum kutoka Umoja wa Mataifa, Interpol, Russia, Marekani na Qatar, na meneja mkuu wa Google kwa masuala ya kijasusi ya kimkakati kukutana.

Kwa ujumla mada ya ya wiki itazungumzia ugaidi kupitia ushirikiano wa kimataifa ulioimarishwa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema wakati wa kikao cha ufunguzi kilichofanyika siku ya Jumatatu, kuwa jambo la msingi ni kuungana sio tu katika kuzuia mashambulizi bali pia kuwa makini na kulenga zaidi kuzuia ugaidi kwa kukapambana na umaskini, ubaguzi, kuboresha miundombinu duni, ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na vichochezi vingine vya msingi.