Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:07

Jeshi la Marekani lashambulia ngome ya Al Shabaab


Kundi la kigaidi la Al-Shabaab nchini Somalia. Picha na shirika la habari la AP
Kundi la kigaidi la Al-Shabaab nchini Somalia. Picha na shirika la habari la AP

Jeshi la Marekani limethibitisha kufanya mashambulizi mapya ya anga dhidi ya wanamgambo wa al-Shabab walioko katika eneo la Middle Juba huko kusini mwa Somalia.

Shambulizi hilo la anga lilifanyika katika mji wa Jilib siku ya Jumamosi kwa kushirikiana na serikali ya Somalia, kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa siku ya Jumatatu na Kamanda wa Marekani kanda ya Afrika inayojulikana kama AFRICOM.

"Tathmini ya awali ya mamlaka hiyo ya kijeshi ni kwamba hakuna raia aliyejeruhiwa au kuuawa," ilisema taarifa hiyo.

Taarifa ya AFRICOM haikusema kama makamanda wakuu wa al-Shabab walilengwa. Wilaya ya Jilib, ni ngome ya al-Shabab na ipo kilomita 385 kusini magharibi mwa Mogadishu.

Shambulio hilo limetokea wakati mkurugenzi wa Shirika la Kitaifa la Ujasusi na Usalama la Somalia, Mahad Salad, alipokuwa Washington na New York, akikutana na maafisa wa Marekani wa Pentagon, CIA na FBI, kwa mujibu wa chanzo kinaichofahamu ziara hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa kutokuwa na mamlaka ya kuzungumza na vyombo vya habari.

Mazungumzo hayo yalilenga katika masuala ya ushirikiano wa kiusalama na kukabiliana na ugaidi kati ya nchi hizo mbili, chanzo hicho kiliongeza.Wakati huo huo, wanajeshi wanne wa serikali ya Somalia waliuawa siku ya Jumatatu katika mlipuko uliotokea kando ya barabara katika wilaya ya Daynile mjini Mogadishu, Wizara ya Ulinzi ilisema.

Brigedia Jenerali Abdullahi Ali Anod, msemaji wa wizara hiyo, alisema kuwa shambulio hilo lilitokea muda wa saa tatu asubuhi, na kwamba wanajeshi watatu na afisa wa kitengo cha ujenzi wameuawa.

Forum

XS
SM
MD
LG