Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:39

UN: Mafuriko katikati mwa Somalia yawakosesha makazi watu 400,000


Mafuriko nchini Somalia.
Mafuriko nchini Somalia.

Mafuriko katikati mwa Somalia yamewakosesha makazi maelfu ya familia huko Beledweyne, mji wenye idadi  kubwa ya watu katika eneo.

Ofisi ya masuala ya kibinadamu ya umoja wa mataifa –OCHA imeripoti kwamba taifa hilo la pembe ya afrika lina zaidi ya watu 460,000 walioathiriwa ikiwemo karibu watu 219,000 waliokoseshwa makazi kwa makadirio ya awali.

Ongezeko la kiwango cha maji Beledweyne kimelazimisha kufungwa kwa msjengo kadhaa muhimu katika mji huo, ikiwemo ofisi na hospitali kuu mjini humo.

Mkazi wa ndani Hussein Yusuf ameliambia shirika la habari la AP kwamba ilikuwa ni mafuriko mabaya kuwahi kutokea ikinukuu uharibifu mkubwa wa mali uliotokea.

Wakaazi wanahofia mlipuko wa ugonjwa wa kipindipindu na Malaria kama mafuriko yataendelea.

Abdifitah Ahmed mkazi wa Beledweyne : “ Ilikuwa ni vigumu kwangu mimi kutembea asubuhi ya leo kwa sababu ya kiwango cha maji. Nilikuwa naweza kutembea zamani, lakini kama unavyoona, maji yamefikia kiunoni kwangu, na hali hii inazidi kuwa mbaya na maji yanayongezeka, na usiku uliopita, iliripotiwa kwamba moja ya nyumba za jirani zangu ilichotwa na maji. Nikitembea katika mtaa huu mara kadhaa leo, jana, na siku moja kabla, leo ni siku mbaya zaidi na kila saa maji yanaongezeka.”

Hussein Yusuf mkazi wa Beledweyne: Mafuriko haya yana tofauti kubwa na mengine yaliyopita. Mafuriko haya ni makubwa kuliko mafuriko mengine katika kumbukumbu ya karibuni ambayo imewahi kutokea kwenye eneo hili. Hata hivyo kwa kuangalia kiwango cha mafuriko, ni lazima pia ikumbukwe kwamba haya ni mafuriko mabaya ambayo hatujawahi kushuhudia.”

XS
SM
MD
LG