Maporomoko ya ardhi yalitokea Jumanne usiku katika kijiji cha Miringati kilichopo eneo la Lubero kwenye jimbo la Kivu Kaskazini, alisema msimamizi wa eneo hilo Edgard Kasombolene.
Kasombolene alithibitisha idadi ya vifo vya watu 10 viliyotangazwa na utawala wa jimbo la Kivu Kaskazini.
Kamanda wa polisi wa eneo la Lubero Kanali Jean Habamungu alisema msako wa kuwatafuta manusura unaendelea siku ya Jumatano.
Maafa haya mapya yanafuatia mafuriko na maporomoko ya ardhi ambayo yaliliathiri eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika siku za hivi karibuni.
Zaidi ya watu 400 wamepoteza maisha wiki iliyopita huko Kivu Kusini, kulingana na idadi rasmi, baada ya mafuriko katika eneo la Kalehe lililoko katika jimbo hilo.
Pia mtu mmoja alifariki siku ya Jumatatu kutokana na maporomoko ya ardhi yaliyotokea katika mgodi wa wachimbaji wadogo wadogo wa Rubaya huko Kivu Kaskazini.
Dozens of armed groups plague eastern Congo, a legacy of regional wars that flared during the 1990s and 2000s.
Wakati huo huo dazeni za makundi yenye silaha yamelikumba eneo hilo la mashariki mwa Congo, mwendelezo wa vita vya kikanda ambavyo vilipamba moto katika miaka ya 1990 na 2000.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP