Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 10:27

Kikosi cha EAC huenda kikaondoka DRC mwezi ujao


Naibu kamanda wa kikosi cha kikanda cha Afrika Mashariki (EACRF) Brigedia Jenerali Emmanuel Kaputa (Kulia) akiwa na msemaji wa kundi la waasi la M23 Willy Ngoma (kushoto) wakipeana mikono huko Kibumba DRC, Desemba 23, 2022. Picha na GLODY MURHABAZI/AFP.
Naibu kamanda wa kikosi cha kikanda cha Afrika Mashariki (EACRF) Brigedia Jenerali Emmanuel Kaputa (Kulia) akiwa na msemaji wa kundi la waasi la M23 Willy Ngoma (kushoto) wakipeana mikono huko Kibumba DRC, Desemba 23, 2022. Picha na GLODY MURHABAZI/AFP.

Kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kilichopelekwa kusaidia kupambana na waasi wa M23, huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huenda kikaondoka mapema mwezi ujao ikiwa hakitatimiza wajibu wake, rais wa DRC Felix Tshisekedi alisema Jumanne.

Kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kilipelekwa nchini humo mwezi Novemba mwaka 2022 ili kusimamia ahadi ya kuondoka kwa M23, kundi la waasi ambalo linadai kuwakilisha maslahi ya kabila la Watutsi, waliopo katika maeneo iliyoyateka miezi nane kabla.

Lakini kuendelea kwa mapigano na M23 kumechangia kuongezeka kwa ukosefu wa usalama katika eneo tete la mashariki mwa Congo, na kusababisha ukosoaji wa mara kwa mara kutoka kwa Tshisekedi kuhusu kikosi cha EAC kutoimarisha kuondoka kwa wanamgambo hao.

Kufuatia mazungumzo kuhusu kumalizika kwa muda wa miezi sita ya mamlaka ya kikosi hicho, Congo imekubali kuongeza muda huo kwa miezi mitatu na kutathmini upya hali hiyo mwezi Juni, Tshisekedi alisema katika hotuba yake wakati wa ziara ya kitaifa nchini Botswana Jumanne jioni.

"Kama muda huo tulioukadiria ukifika, na agizo halijatimizwa, basi tunaweza kuamua kupeleka kikosi kingine," alisema.

Msemaji wa kikosi cha EAC alikataa kutoa maoni na alielekeza maswali kwa katibu mkuu wa EAC, Peter Mathuki, ambaye hakuweza kupatikana mara moja.

Uwezekano wa kuondoka kwao kunaweza kutabiri kuwasili kwa kikosi tofauti kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).
Siku ya Jumatatu, katika kilele cha mkutano usiso wa kawaida SADC iliidhinisha kupelekwa kwa kikosi kama hicho ili kusaidia kurejesha usalama mashariki mwa Congo, lakini hakikutoa tarehe ya kuwasili kwao.

Chanzo cha bahari hii ni Shirika la habari la Reuters.

XS
SM
MD
LG