Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 01:47

Rais Tshisekedi akosoa utendaji kazi wa kikosi cha wanajeshi wa Afrika mashariki


Wanajeshi wa Kenya wanaoshiriki katika kikosi cha Jumuia ya Afrika mashariki kilichopelekwa mashariki mwa DRC.
Wanajeshi wa Kenya wanaoshiriki katika kikosi cha Jumuia ya Afrika mashariki kilichopelekwa mashariki mwa DRC.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi Jumanne amekikosoa kikosi cha wanajeshi waliopelekwa na mataifa ya Afrika Mashariki kurejesha hali ya utulivu katika eneo lenye mzozo la Mashariki mwa Congo, akidokeza kwamba wanajeshi hao wanaweza kuondoka mwishoni mwa mwezi Juni.

Akizungumza wakati wa ziara yake nchini Botswana, Tshisekedi alielezea wasiwasi wake kuhusu “kuishi pamoja” kati ya waasi na kikosi hicho cha Afrika Mashariki ambacho kilianza kupelekwa DRC mwishoni mwa mwaka jana.

Makundi mengi yenye silaha yanavuruga usalama Mashariki mwa DRC.

Kundi la M23, limeanzisha mashambulizi tangu lilipoibuka tena baada ya kusambaratika mwishoni mwa mwaka 2021.

Jumuia ya Afrika Mashariki yenye nchi wanachama saba iliunda kikosi cha kijeshi kukabiliana na mzozo mwezi Juni mwaka jana, huku wanajeshi wa Kenya wakipelekwa mwezi Novemba wakifuatiwa baadaye na wanajeshi wa Burundi, Uganda na Sudan Kusini.

“Kuna kuishi pamoja ambako tumeona kati ya kikosi cha Jumuia ya Afrika Mashariki na waasi,” Tshisekedi alisema katika mkutano na waandishi wa habari.

“Hilo ni tatizo la kweli linapokuja suala la jukumu kikosi hicho kilipangiwa kazi na pia inapelekea kuuliza, nini madhumuni ya kikosi hicho? Alisema, akidai kuwa isipokuwa wanajeshi wa Burundi, wengine sasa wanaishi pamoja na waasi wa M23”.

Ametoa maoni hayo siku moja baada ya mkutano maalum wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika nchini Namibia, ambao uliazimia kupeleka wanajeshi “kurejesha amani na usalama” Mashariki mwa DRC.

XS
SM
MD
LG