Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 10:30

Mapigano mapya yazuka Mashariki mwa DRC


Wanajeshi wa DRC wapelekwa katika eneo lililoshambuliwa na waasi wa M23. Picha na mwandishi wa VOA Austere Malivika
Wanajeshi wa DRC wapelekwa katika eneo lililoshambuliwa na waasi wa M23. Picha na mwandishi wa VOA Austere Malivika

Mapigano mapya kati na waasi wa M23 yalizuka Jumatano karibu na mji wa Goma ulioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kulingana na maafisa, na kuvuruga wiki kadhaa za utulivu ambao ulishuhudiwa katika eneo hilo ambalo limekumbwa na machafuko.

Kundi la M23 linaloongozwa na Watutsi, limekuwa likipata ushindi mfululizo dhidi ya jeshi na makundi hasimu ya wanamgambo tangu lilipoibuka tena mwishoni mwa mwaka 2021, na kuteka maeneo ya jimbo la Kivu Kaskazini.

Kundi hilo pia limesababisha mzozo mkubwa wa kibinadamu wakati lilipoufunga mji mkuu wa jimbo, Goma, kitovu cha biashara chenye watu zaidi ya milioni moja.

Jumatano asubuhi, watu wenye silaha wanaodai kuwa wazalendo wa Congo walishambulia maeneo yanayokaliwa na M23 yaliyopo karibu na Kibumba, takriban kilomita 20 (maili 12) kaskazini mwa Goma, kulingana na afisa wa jeshi ambaye aliomba jina lake lisitajwe.

Wapiganaji wa M23 walidhibiti mashambulizi hayo na baadaye jeshi hilo likawakamata washambuliaji, afisa huyo wa jeshi aliongeza.

Fataki Sebatutsi kiongozi wa jamii ya kiraia katika eneo la Kibumba, pia aaliliambia shirika la habari la AFP kuhusu kutokea kwa mapigano hayo.

Kiongozi wa kundi la M23 Bertrand Bisimwa alitweet siku ya Jumatano kuwa "muungano wa serikali ya Kinshasa" umeshambulia maeneo yake.

Hali ya utulivu ilikuwa ilitawala kwa wiki kadhaa kabla ya shambulio hilo, huku wanajeshi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakipeleka majeshi katika eneo hilo kwa lengo la kusimamia mpango uliokusudiwa wa kujiondoa kwa M23.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.

XS
SM
MD
LG