Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 00:51

Watu 20 wameuawa mashariki mwa DRC na kundi linaloshutumiwa waasi wa ADF


Ghasia zilizofanyika hivi karibuni huko Beni nchini DRC na kupelekea vifo pamoja na uharibifu wa mali za raia
Ghasia zilizofanyika hivi karibuni huko Beni nchini DRC na kupelekea vifo pamoja na uharibifu wa mali za raia

Mukohe alisema alihesabu miili 21 ya wanaume na wanawake kwenye eneo la mauaji kiasi cha kilomita 30 magharibi mwa mji wa Oicha katika jimbo la Kivu Kaskazini

Kiasi cha watu 20 wameuawa katika shambulizi huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo huku vyanzo vikiwalaumu waasi wenye uhusiano na kundi la jihadi la Islamic State. Adui Allied Democratic Forces (ADF) waliwashambulia wakulima majira ya saa kumi jioni siku ya Ijumaa karibu na kijiji cha Enebula alisema kiongozi wa kiraia katika eneo Patrick Mukohe aliiambia AFP.

Mukohe alisema alihesabu miili 21 ya wanaume na wanawake kwenye eneo la mauaji kiasi cha kilomita 30 magharibi mwa mji wa Oicha katika jimbo la Kivu Kaskazini. Wakati huo huo Jules Kambale ambaye anafanya kazi katika chumba cha kuhifadhi maiti kwenye hospitali ya Oicha alisema alipokea miili 19.

Charles Ehuta Omeanga, kiongozi wa jeshi kikanda alithibitisha shambulizi hilo ambalo alielezea kuwa la magaidi wa ADF, lakini alisema hayuko katika nafasi ya kutaja idadi kamili ya vifo. ADF kiasili ni waasi kutoka nchini Uganda ambao wameingia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo katika miaka ya 1990 na tangu wakati huo wanashutumiwa kuua maelfu ya raia na kupelekea mauaji makubwa kufanywa na kikosi hicho katika eneo.

Tangu mwaka 2019 baadhi ya mashambulizi ya ADF mashariki mwa DRC yamekuwa yakidaiwa kufanywa na Islamic State, ambalo linasema kundi hilo kama eneo lake la ndani, The Islamic State Central Africa Province. Katika video iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii na kuthibitishwa na Mukohe umati wa watu umeuzunguka mwili wa mtu aliyefungwa kwenye fremu ya mbao na koo lake limekatwa.

XS
SM
MD
LG