Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:27

Uganda yatuma wanajeshi zaidi kuwafuatilia waliowauwa wanafunzi 37


Maziko ya wanafunzi waliouawa na Waasi nchini Uganda.
Maziko ya wanafunzi waliouawa na Waasi nchini Uganda.

Mamlaka nchini  Uganda imesema imewakamata watu watatu waliohusika na shambulizi katika shule Ijumaa ambapo takriban watu 40 waliuwawa.

Waathirika wengi ni wanafunzi katika shule ya Lhubiria katika mji wa magharibi- Mpondwe.

Wengi walichomwa moto hadi kufa katika bweni lao.

Kamishna wa wilaya Joe Walusimbi amesema watu waliokamatwa ilitokana na vidokezo kutoka kwa wakaazi wa eneo hilo.

Rais wa Uganda Joweri Museveni Jumapili aliamuru kupelekwa wanajeshi zaidi magharibi mwa uganda ambako washambuliaji kutoka kundi lenye uhusiano na Islamic State wamewauwa wanafunzi 37 katika shule ya sekondari.

Wanachama wa kundi la uasi la ADF waliwauwa wanafunzi ijumaa usiku katika shule ya sekondari ya Lhubirira huko Mpondwe karibu na mpaka wa jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.

Jeshi na polisi wamesema washambuliaji pia waliwateka wanafunzi sita na kukimbilia kuelekea mbuga ya wanyama pori ya Virunga upande wa pili wa mpaka.

Washambuliaji wamesababisha ukosoaji mkubwa wa kimataifa ikiwemo kutoka Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na shirika la maendeleo la serikali za nchi za Afrika. Uganda ilishtushwa na shambulizi hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG