Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 06:07

Wanafunzi 41 wauawa nchini Uganda katika shambulio la ADF


Mwanafunzi asaidiwa na mzazi kwenye shule iliyoshambuliwa na wanamgambo wa ADF huko Mpondwe, Uganda.
Mwanafunzi asaidiwa na mzazi kwenye shule iliyoshambuliwa na wanamgambo wa ADF huko Mpondwe, Uganda.

Wanamgambo wa kundi la ADF wenye uhusiano na kundi la Islamic State waliua wanafunzi 41 na kuteka nyara wengine sita katika shambulio kwenye shule kaskazini mwa Uganda karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, jeshi lilisema Jumamosi.

Wanajeshi walipata miili ya waliokufa walipofika shuleni, msemaji wa jeshi Felix Kulayigye alisema katika taarifa.

Kulayigye alisema mapema Jumamosi kwenye Twitter “Jeshi lilikuwa linamsaka adui ili kuwaokoa waliotekwa nyara na kuangamiza kundi hilo.”

Maafisa wa polisi na jeshi wanasema washambuliaji walikua watano na walitia moto bweni baada ya kupora chakula na vitu vingine .

Polisi walisema washambuliaji kutoka kundi la ADF walikimbia kuelekea mbuga ya Virunga nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kituo cha Televisheni cha kibinafsi, NTV Uganda kilisema kwenye Twitter kwamba idadi ya waliofariki ilifikia 41, huku gazeti la serikali la New Vision likisema waliouawa ni 42.

New Vision ilisema 39 kati ya waliofariki ni wanafunzi, na kwamba baadhi ya waliouawa walikufa wakati washambuliaji walipotega bomu wakati wakikimbia.

Forum

XS
SM
MD
LG