Taarifa ya jeshi ilisema shambulizi hilo lilitokea katika wilaya mpakani ya Kech kwenye jimbo la Baluchistan.
Wanajeshi wa Pakistani walijibu mashambulizi hayo “kwa silaha zote zilizokuwepo” na kuwafurusha washambuliaji hao kufuatia mapambano yaliyohusisha silaha nzito, iliongeza.
“Majeshi ya usalama yamefanya operesheni ya kusafisha eneo hilo na wanawasiliana na mamlaka nchini Iran upande wa pili pia kuzuia fursa ya magaidi hao kukimbia,” taarifa hiyo ilisema.
Hakuna madai ya mara moja kuhusu kundi hilo kuhusika na shambulizi hilo la kikatili.
Katika ujumbe wake wa Twitter, Ubalozi wa Iran mjini Islamabad ulisema “unalaani vikali shambulizi hilo la kigaidi” na kutuma rambi rambi kwa familia za wanajeshi waliouawa.
Ubalozi huo ulisisitiza haja ya kuwepo “ushirikiano wa pande mbili” katika kupambana na ugaidi, na kusema “ni maumivu ya pamoja.”
Wiki iliyopita, Tehran ilisema shambulizi la “kigaidi” liliuua wana usalama wa Iran sita katika upande wa mpaka wake na Pakistan, ikidai kuwa washambuliaji hao walikuwa wanajaribu kuingia Iran na walitoroka wakiwa na majeraha.
Islamabad ililaani shambulizi hilo na kutaka juhudi za pamoja zichukuliwe kuwafurusha magaidi pande zote mbili za mpakani.
Nchi zote zimeendelea kulaumiana kuwa hazichukui hatua za kutosha kuwazuia wanamgambo kutafuta hifadhi katika nchi hizo na kuanzisha mashambulizi ya kuvuka mpakani.
Forum