Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 13:11

Wanajeshi 6 na raia mmoja wauwawa katika mapigano Pakistan

Mlipuko wa bomu Pakistan.(AP)
Mlipuko wa bomu Pakistan.(AP)

Maafisa wa Pakistani wamesema Jumamosi kwamba mapigano ya usiku na magaidi katika jimbo la kusini maghararibi la Baluchistan yalisababisha vifo vya wanajeshi sita na raia mmoja, pamoja na washambuliaji sita.

Wengine sita walisemekana kujeruhiwa.

"Katika mchakato wa operesheni ya kusafisha, watu 7 ikiwa ni pamoja na raia mmoja ambao walikuwa wamekumbatia dhana ya kufia dini wameuwawa wakati wengine 6, ikiwa ni pamoja na mwanamke mmoja wamejeruhiwa," tawi la habari la kijeshi, Inter-Services Public Relations, lilisema.

Ghasia hizo zilizuka siku ya Ijumaa jioni wakati wanamgambo wenye silaha za kivita walivamia kambi kuu ya wanajeshi takriban kilomita 100 kaskazini mwa mji mkuu wa jimbo wa Quetta, ISPR ilisema.

XS
SM
MD
LG