Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 06:47

Afisa wa WHO aliyejitoa mhanga kuwasaidia wakimbizi wenzake auawa


Wanawake wa Kisomali wakiwahudumua watoto wao wanaokabiliwa na utapiamlo Agosti 15, 2011. Picha na ROBERTO SCHMIDT / AFP.
Wanawake wa Kisomali wakiwahudumua watoto wao wanaokabiliwa na utapiamlo Agosti 15, 2011. Picha na ROBERTO SCHMIDT / AFP.

Nasra Abdi Hassan, alikua mmoja wa maafisa wa afya ya jamii katika Shirika la Afya Duniani, WHO, aliwasili Mogadishu asubuhi ya tarehe 9 mwezi June kuhudhuria mafunzo ya kuwahamisha wanawake juu ya umuhimu wa usalama wao.

Baadaye siku hiyo, alienda kwenye hoteli nzuri ya Lido Pearl Beach kwa ajili ya chakula cha jioni na rafiki yake. Majira ya saa 7:55 usiku, wanamgambo wa al-Shabab waliishambulia hoteli hiyo. Hassan alikuwa mmoja wa raia sita waliopigwa risasi na kuuawa.

Kifo cha mtu aliyehamia nchi ya asili walikotoka mababu zake kutoa huduma ya afya kilikua kitendo kilichovunja moyo na kuwatia huzuni kubwa wakimbizi wengi wa Somalia. Alithubutu kwenda Somalia wakati maelfu ya Wasomali wamesalia Kenya wakiwa wakihisi kutokuwa salama na wana wasiwasi kurejea nyumbani.

"Sikufurahia kurudi kwake," anasema babake, Abdi Hassan. "Yeye na mama yake walinizidi nguvu. Niliwaambia, 'Msihatarishe maisha yake kwa dola mia kadhaa. Tutapata chakula."

Hassan alizaliwa na kukulia Dhagahley, moja ya kambi za wakimbizi za Dadaab nchini Kenya. Familia yake ilitumia kila walichoweza kumudu kumpeleka shule jijini Nairobi na kusaidia kuendeleza masomo yake ya juu. Alikuwa mwanafunzi mzuri. Alipata diploma ya masomo ya virutubisho na lishe kutoka Chuo Kikuu cha Mount Kenya.

Miaka miwili iliyopita, alisafiri hadi Afmadow katika jimbo la Jubaland nchini Somalia na kufanya kazi inayohusaiana na afya ya wanawake katika shirika hilo lisilo la kiserikali la .

Mwaka jana, aliteuliwa kama afisa wa afya ya jamii wa wilaya ya Afmadow, akifanya kazi ya kusaidia oparasheni zinayokabiliana na ukame za WHO.

Baada ya kupigwa risasi, WHO iliandika tweet ya kumkumbuka Hassan, ambaye alikuwa na umri wa miaka 27.

"Alichukua majikumu makubwa katika kuunga mkono oparesheni ya kukabiliana na ukame huko Jubaland na kuwatia moyo watu wengi kwa kujitoa kwake bila kuyumbayumba," ofisi ya WHO Somalia iliandika kwenye ukurasa waTwitter.

Fardawsa Sirad Gelle, aliyezaliwa mwaka mmoja na Hassan huko Dadaab, anasema kifo cha Hassan kinakumbusha kwamba kungali na hatari kubwa nchini Somalia.

Forum

XS
SM
MD
LG