Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 05:34

Siku ya Wakimbizi Duniani yadhimishwa ikiwa na changamoto nyingi


Watoto wakimbizi kutoka Sudan Kusini wanaendesha baiskeli zao katika makazi ya wakimbizi ya Palorinya, Uganda. Oktoba 25, 2017. Picha na REUTERS/James Akena
Watoto wakimbizi kutoka Sudan Kusini wanaendesha baiskeli zao katika makazi ya wakimbizi ya Palorinya, Uganda. Oktoba 25, 2017. Picha na REUTERS/James Akena

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi linaadhimisha Siku ya Wakimbizi Duniani mwaka huu kwa ujumbe kwamba "kila hatua ni muhimu".

Katika siku hii dunia inaendelea kukabiliwa na changamoto zilizotokana na janga la COVID-19 na ikiwa na idadi kubwa ya watu waliolazimika kuyahama makazi yao kutokana na vita pamoja na hali mbaya ya hewa.

Migogoro, njaa na misukosuko ya kiuchumi imewakosesha makazi takrikan watu milioni 80 duniani kote, nusu yao wakiwa watoto, ilipofika mwishoni mwa mwaka 2019—idadi iliongezeka karibu mara mbili ya idadi ya muongo uliopita.

Katika bara la Afrika peke yake, mapigano huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burkina Faso na eneo la Sahel yamechangia katika idadi ya wakimbizi kuongezeka hadi milioni 6.3, Clementine Nkweta-, mkurugenzi wa UNHCR kwa Afrika Mashariki, Pembe ya Afrika na Maziwa Makuu alisema.

"Mtu mmoja kati ya kila watu 97 huhamishwa kwa nguvu. Katika bara (la Afrika), na tunaona idadi ikiongezeka. Tuliuanza muongo kukiwa na kiasi cha watu milioni 2.2 na idadi hiyo imeongezeka takriban mara tatu.” alisema Salami.

Moshi ukifuka juu ya majengo kusini mwa jiji la Khartoum, wakati mapigano yakiendelea Mei 16 2023. Picha na AFP.
Moshi ukifuka juu ya majengo kusini mwa jiji la Khartoum, wakati mapigano yakiendelea Mei 16 2023. Picha na AFP.

Mwaka huu, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, linakadiria kuwa watu milioni 117.2 wakimbizi watakoseshwa makazi kwa nguvu au wasiokuwa utaifa wataondoka kwenye makwao kwa sababu mbalimbali wakikimbia maeneo mengine duniani.

Katikati ya mwezi Aprili mwaka huu, Sudan imekuwa uwanja wa vita, kutokana na mzozo mkali wa kati ya majenerali wawili Sudanese Armed Forces (SAF) na Rapid Support Forces (RSF) wanaogombea madaraka, mzozo ambao umewalazimisha watu kuyahama makazi yao hali hii inaendelea kuongezeka.

Katika miaka ya hivi karibuni nchi saba majirani na Sudan, tano kati yao - Ethiopia, Chad, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Libya na Sudan Kusini - pia zimepitia migogoro na machafuko ya kisiasa.

Sudan iliwahi kuwa mwenyeji wa zaidi ya wakimbizi milioni moja, ikiwa ni nchi ya pili kuwa na idadi kubwa ya wakimbizi barani Afrika.

Hivi sasa, maelfu ya wakimbizi wanahamishwa tena, wengine wanalazimika kurudi kwenye machafuko yale yale waliyokimbia hapo awali. Kwa mfano, nchini Chad, moja ya nchi maskini sana duniani, ongezeko la ghafla la idadi ya watu nchini humo limesababisha ongezeko bei ya vyakula.

Baadhi ya habari hii imetoka Shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG