Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:47

Misri kupatiwa dola milioni 22 kukabiliana na wimbi la wakimbizi wa Sudan


 Josep Borrell
Josep Borrell

Mkuu wa sera wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell ametangaza kutolewa fedha dola milioni 22 kwa ajili ya kusaidia serikali ya Misri kutokana na wimbi kubwa la wakimbizi kutoka Sudan waliokimbia vita na kukatisha kuingia Misri.

Tangazo la Borrell limekuja wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari Mjini Cairo na waziri wa mambo ya nje wa Misri Sameh Shoukry.

Kwa mujibi wa shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, Misri imepokea zaidi ya wakimbizi laki mbili kutoka Sudan tangu mapigano yalipozuka katikati ya mwezi Aprili.

Borrell pia ameelezea suala la wahamiaji baada ya boti moja kuzama kwenye ufukwe wa Ugiriki na kuua watu 79 na wengi wakiwa hawajulikani walipo katika janga kubwa na baya kutokea mwaka huu.

Borrell amesema EU imetoa Euro 80 milioni kwa ajili ya udhibiti wa mpakani, kusaka na kuokoa na kuendesha operesheni za kupambana na magendo. Shoukry amesema msaada zaidi ni muhimu ili kudhibiti suala hili.

Josep Borrell mwakilishi wa juu wa EU kwa ajili ya maswala ya kigeni na sera za usalama.

“katika siku chache, zaidi ya watu laki mbili wamepokelewa misri na ni lazima niwashukuru kwa jaili hiyo , umoja wa ulaya utatoa msaada wa haraka wa dola milioni 22, kuwasaidia nyie kushughulika na wimbi hili jipya la wakimbizi kutoka sudan katika mpaka wenu wa kusini. Najua hazitoshi, najua mtalipa zaidi , lakini angalau , wacha na sisi tuchangie kidogo katika msaada wenu.’

Forum

XS
SM
MD
LG